Saratani ya shingo ya kizazi ni saratani ambayo hutokana na mabadiliko ya mfumo wa chembechembe au cells zilizoko katika shingo ya kizazi.Mabadiliko haya hupelekea chembe chembe hizo kushamiri na kuzaliana kwa kasi kinyume na mpangilio wa maumbile.
Saratani ya Shingo ya kizazi yasemekana kuwa ni saratani ya nne inayoongoza kwa kusababisha vifo vya wanawake katika nchi zinazoendelea. Repoti ya 2012 ya shirika la afya duniani 'WHO' imesema kati ya matukio 75,000 ya waathirika wa saratani ya kizazi barani Afrika, 50 ,000.Namba za matukio haya zinawakilisha waathirika waliopata fursa ya utafiti.
NINI KISABABISHACHO SARATANI YA SHINGO YA UZAZI ?
Ripoti za utafiti wa kisayansi zimeafiki kuwa asilimia 99% ya saratani za shingo ya kizazi hutokana na maambukizi ya virusi vya 'Human Papillomavirus' au HPV vilivyoko katika jamii ya papilloma. Baadhi ya virusi hivi vyenye aina zaidi ya mia moja huambukizwa kwa njia ya kujamiana.
BAADHI YA MAMBO YANAYOONGEZA HATARI ZA KUPATA SARATANI YA SHINGO YA KIZAZI?
Kushiriki tendo ndoa katika umri mdogo au chini ya miaka 18Kuwa na wenzi tofauti au mwenzi aliye na wapenzi tofautiUtumiaji wa sigara kwani hupunguza nguvu ya kinga mwilini(impairs immune system)Watu wenye kinga hafifu ya mwili au magojwa kama UkimwiUzazi wa mara kwa mara
Saratani ya shingo ya kizazi
January 03, 2023